Yajapo ni mambo yanapokuja na Yapokee ni kukubaliana nayo.
Category Archives: Afya ya akili
Wakati Ni Upepo
Ya kale ni mambo ya zamani, ambayo yamepita muda mrefu. Unaposema hayanuki, ina maana gani? Hebu tuchukue mfano wa kinyesi cha ng’ombe. Endapo kinyesi hicho ni cha kale ama cha zamani huwa hakitoi harufu kwa sababu kinakuwa kimekauka.
Maamuzi Yako Ya Leo Matokeo Ya Kesho
Maamuzi ni neno linalotokana na neno amua au kata shauri. Matokeo ni jibu au jawabu. Hivyo msemo huu una maana kwamba unavyoamua leo ni jibu la kesho yako. Hapa tunakumbushwa kuwa yatupasa tuwe na maamuzi mazuri ya leo ili yawe jawabu lako zuri la kesho.
Chaka La Simba Halali Nguruwe
Chaka ni mahali ambapo pana miti mingi lakini pia na nyasi ndefu zinakuwepo. Mahali hapa ndio maficho mazuri kwa simba.
Ya Kale Hayanuki
Ya kale ni mambo ya zamani, ambayo yamepita muda mrefu. Unaposema hayanuki, ina maana gani? Hebu tuchukue mfano wa kinyesi cha ng’ombe. Endapo kinyesi hicho ni cha kale ama cha zamani huwa hakitoi harufu kwa sababu kinakuwa kimekauka.
Uvaaji Wako Unakutambulisha Ulivyo
Uvaaji ni neno litokanalo na neno kuvaa. Kutambulisha ni kufahamika au kukupa utambulisho wa aina fulani. Nguo ni mavazi yanayovaliwa ili kusitiri maungo ya mwanadamu.
Dawa Siyo Kama Chumvi
Dawa ni aina ya tiba itumikapo tunapougua, hupewa na madaktari ili tujitibie kulingana na maelekezo yao. Chumvi ni kiungo muhimu cha chakula. Kiungo hiki ni cha lazima kuliko viungo vyote ambavyo hufanya chakula kuwa na ladha nzuri.
Elimu Ni Mali
Elimu ni maarifa, ujuzi na uelewa tuupatao kutokana na kusoma. Elimu siyo kitu ambacho mtu anazaliwa nacho. Ukiwa na kipaji cha kuzaliwa nacho huweza kuongezewa kwa kusoma zaidi.
Maneno Matupu Hayavunji Mfupa.
Maneno ni matamshi yaliyoandikwa ama yaliyotamkwa kutoka kwenye vinywa vya watu. Mathalani, maneno yanaposemwa juu yako ni budi ukayatafakari kwanza ili ujue yana maana gani. Endapo maneno hayo hayaleti madhara yoyote basi hayatakuwa na shida kwako, shida itakuwa pale tu mtu atakapokushikia silaha na akakudhuru.
Ubaya Ni Deni Linalosubiriwa Kulipwa
Ubaya ni ile hali ambayo mtu humfanyia mwingine jambo ambalo sio la kiungwana. Inawezekana ubaya huo unafanyika kwa ajili ya kumrudisha mtu nyuma kwa kile alicho nacho. Hiyo ni roho ya kwa nini na chuki kwa mwingine. Lakini ikumbukwe kuwa unapofanya ubaya kwa mwingine lazima nawe itafika muda ambao utatendewa vile vile au hata zaidi ya vile. Mara nyingi huwa tunasahau kuwa amtendeaye mwenzie naye atatendewa sawasawa na vile alivyomfanyia mwenzake.